TIZAMA VIDEO:Mayahudi wajiandaa kuivamia mji wa Ghaza

Saturday July 05, 2014 - 21:39:30
10360
Super Admin
Maelfu ya wanajeshi wa Kiyahudi waliojihami na silaha pamoja na Magari ya kivita wamekaribia kuingia mji wa Ghaza na wametishia kuingia kwa nguvu mji huo.





Habari kutoka mji wa Ghaza katika Ardhi ya Waislaam wa Falastine zinaeleza kuwa Makundi yote ya kijihadi katika mji wa Ghaza wamewekwa kwenye hali ya tahadhari.





Waziri mkuu wa Israel Binyamin Netenyahu amezungumza na vyombo vya habari na kuwaamuru Wanajeshi wake kuelekea upande wa Ghaza ili kwenda kufanya mauaji dhidi ya Wananchi wa Kislaam wa Falastine.




Mayahudi wanajaribu kufanya mauaji mengine dhidi ya waislaam wa falastine baada ya kutekwa Mayahudi 3 katika siku za hivi karibuni kwenye mji wa Alkhalil na baadae kuawa.




Kikosi cha Izzudiin Qasam cha Wanajeshi wa Hamas imetangaza kujiandaa kuwazuia Wanajeshi wa Kizayuni wa Israel walio na lengo la kufanya mauaji ya waislaam wa Ghaza.





Msemaji wa Izzudiin Qasam aliyezungumza na vyombo vya habari amesema Wanajeshi wao wako tayari kukabiliana na uvamizi wa kiadui wa Wanajeshi wa Israel dhidi ya mji wa Ghaza.




Wapiganaji wa Mujahidina waliofunga nyuso zao na waliojihami na silaha walionekana wakifanya maonyesho ya kijeshi katikati mwa mji wa Ghaza.





Kundi lingine la Mujahidina nao wamefanya maonyesho ya Kijeshi na kutangaza hali ya tahadhari na kuwaambia wananchi wa Kislaam kuwa tayari kukabiliana na Maadui hao wa Israel.




Kundi la Jihadul Islami nae limeonyesha uwezo wake wa Kijeshi makundi yote ya Kijihadi kwenye Ardhi ya Falastine wametangaza hali ya tahadhari na pia kuwahimiza Waislaam wa Ardhi hiyo kukabiliana dhidi ya Uvamizi wa Mayahudi.





Vijana wanaosoma kwenye Vio Vikuu na Mashule wamesema wanashiriki kulinda Mji wa Ghaza Dhidi ya Uvamizi wa Mayahudi,hali katika mji wa Hali ni ya Kivita zaidi.




Afisa aliyezungumza kwa niaba ya Utawala wa Israel amesema Jeshi lao halina maslahi wa kuingia upande wa Mashariki mwa Ghaza ila ameongeza kusema kuwa ni kutaka kupunguza uwezo wa Makundi aliyowaita kuwa ni Makundi ya Kigaidi akiwa na maana kwa Makundi ya Kijihadi ya Falastine.


TIZAMA VIDEO HAPA CHINI KWA MFUMO WA YOUTUBE




Related Items

Update cookies preferences