UFAFANUZI:Maaskari 3 na Afisa mmoja waliouawa katika mji wa Mugadishu.

Monday July 07, 2014 - 23:55:41
7807
Super Admin
Watu waliojihami na Silaha wamefanya mauaji tofauti tofauti dhidi ya Maofisa na Maaskari wa Serikali ya FG katika mji wa Mugadishu nchini Somalia.




Wilaya ya Wadajir ameuliwa Askari mmoja wa kijeshi na mwingine kujeruhiwa vibaya,shambulio lingine limetokea katika makutano ya Barabara ya Tawfiq Wilayani Yaqshiid na ameuawa mmoja wa maofisa wa Usalama wa Serikali ya FG,Shuhuda aliykuwepo eneo la tukio amenukuliwa akisema kuwa afisa huyo aliyeuawa alikuwa na Gari aina ya Raada.




"Watu waliokuwa na silaha walimwua Askari mmoja wa Serikali ya FG katika mtaa wa Tawfiiq Wilayani Yaqshiid,kifo chake ilikuja baada ya kushuka kutoka kwenye Gari yake na kujaribu kuingi Nyumba ya babake aliyeuawa",alisema Shuhuda huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.





Upande mwingine watu waliojihami na silaha walimpiga risasi Askari mmoja wa Serikali ya FG na kisha kuchukua Bunduki lake la AK47 na kutoweka nalo kusikojulikana,mauaji haya Askari huyo ilifanyika mtaa wa Biya Wilayani Sukha Holaha,pia Askari mwingine ameuawa jana usiku katika mtaa wa SISI Wilayani Yaqshiid Mkaoni Banadir.




Mahad Yare


SomaliMemo,Mugadishu


Related Items

Update cookies preferences