Serikali ya FG na Wanajeshi wa AMISOM waudhibiti upya Ikulu baada ya kutekwa na Al-Shabab.

Wednesday July 09, 2014 - 10:45:58
8663
Super Admin
Baada ya masaa sita mfululizo ya mapigano makali yaliofanyika ndani ya Majengo ya Ikulu ya Rais wa Serikali ya FG hatimae Serikali wakishirikiana na Wanajeshi wavamizi wameudhibiti upya kwenye majengo hayo ya Ikulu.



Habari kutoka kwenye Jumba hilo linalojulikana Villa Somalia zinaeleza kuwa Wanajeshi wa AMISOM wakiwa na Vifaru na Magari mengine ya Kivita wanafanya Doria katika eneo la Ikulu.




Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa Makumi ya Maaskari na Maofisa wa Serikali ya FG wameuawa kwenye Mapigano ya jana usiku ambapo athari yake ilisikika hadi kwenye Wilaya zilizo mbali na IKULU.




Maofisa wa Polisi na yale ya Kijeshi walifika eneo la Mapambano na kuanza uchunguzi,Baadhi ya Viongozi akiwemo Hassan Sheikh na Waziri mkuu wamerudi upya baada ya jana usiku kukimbizwa Kambi kuu ya Wanajeshi wa AMISOM ya Halane.




Nicholas Kay ambae ni mjumbe maalum wa U.N nchini Somalia anatarajia kutoa taarifa rasmi kuhusiana mapigano makali yalioitikisa mji wa Mugadishu jana usiku.




Harakat Al-Shabab Al Mujahideen nao kwa upande wao wanatarajiwa kutoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na Uvamizi wa Ikulu jana usiku kama ilivyodai vyanzo vya habari mjini Mugadishu.




Liban Jehow Abdi


SomaliMemo,Mugadishu


Related Items

Update cookies preferences