Utawala wa Libya yaiomba U.N kutuma Wanajeshi kwa nchi hiyo.

Wednesday July 16, 2014 - 23:34:44
7639
Super Admin
Waziri wa masuala ya nje wa Libya amesema ameiomba Umaoja wa Mataifa kuingilia kati kijeshi katika nchi hiyo.




Wanamgambo waliokuwa wamejihami na Silaha siku chache zilizopita walipigana ndani ya Uwanja wa Ndege wa mji wa Tripoli na kuakhirishwa kazi zote za Uwanja huo.





"Libya inaiomba Umoja wa Mataifa kuingilia Kijeshi Taifa hili ili kuiokoa Serikali na Taifa kwa ujumla ambayo iko hatarini",alisema Waziri huyo wa Masuala ya Kimataifa wa Libya.




Waziri mkuu wa mpito wa Libya nae kwa upande wake amesema kwa yeye Binafsi anafikiri kwenda kumwomba Bankii Muun uingiliaji wa Kigeni kwa Libya.




Mapigano yaliodumu masaa kadhaa yaliharibu makumi ya Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Libya na kwenye miji mikubwa wa nchi hiyo Wafanykazi wote wa Kigeni wamehamishwa.




Mji wa Benghazi kuna Makabiliano makali kati ya Mujahidina wa Ansaru Sheria na Wanamgambo wa Khalif Haftar ambae ni mhalifu wa Kivita anaetumiwa na Amerika na Mataifa ya Magharibi.

Related Items

Update cookies preferences