Wanajeshi wa Kislaam wautwaa miji 3 bila mapigano ndani ya Mkoa wa Lower Shabelle nchini Somalia.

Friday July 04, 2014 - 00:30:37
11007
Super Admin
Vikosi vya Mujahidina wa Al-Shabab.
Vikosi vya Mujahidina wa Al-Shabab.
Habari kutoka mkoa wa Lower Shabelle zinaeleza kuwa kuna mabadiliko upande wa ki Utawala baadhi ya Wilaya zilizopo kwenye mkoa huo.





Vikosi vya Mujahidina wa Wilayatul Islamiah ya Lower Shabelle wameutwaa Baadhi ya Wilaya 3 zilizo karibu sana na Buurhakaba,vyanzo muhimu vya kuaminika vinaeleza kuwa Vikosi vya Mujahidina tayari wameweka kambi zao kwenye miji ya Jiira-Kuuloow,Qardo,na Jama'a.




Wanamgambo waliokuwa wakiunga mkono Serikali ya FG ambapo katika miezi ya hivi karibuni walikuweko kwenye eneo la Barabara ya Lami inayounganisha kati ya Balidoogle na Buurhakaba wamejiondokea kutoka miji hizo.




Mamia ya Wanajeshi wa Al-Shabab wameelekea upande wa Barabara ya Lami na Wanamgambo waliokuwa wameweka Beria kwenye Barabara hiyo wametorokea upande wa Lego kama walivyonukuliwa na Wakaazi.





Kamanda wa Jeshi la FG amethbitisha hatua hiyo na kusema kuwa Wanajeshi wake wametoka kutoka Miji mitatu kwa kile alichokitaja kuwa ni Mpango wa Kivita na Kukosa msaada wa kijeshi kutoka kwa upande wa AMISOM.





Wasafiri waliokuwa wakisafiria kwenye Barabara inayounganisha kati ya Mugadishu na Baydoba wamesema wamewaona Vikosi vya Mujahidina wa Al-Shabab wakifanya ukaguzi kwenye Magari za Raia.





Liban Jehow Abdi



SomaliMemo,Mugadishu



Related Items

Update cookies preferences