Ni nani Sheikh Mohamed Idrisa aliyeuawa jana mjini Mombasa?

Wednesday June 11, 2014 - 11:15:56
14745
Super Admin
Wakati hali ya usalama kwenye miji mbalimbali nchini Kenya ukidorora mauaji ya kupangwa yamendelea kuongezeka kwenye Miji hizo.
Habari kutoka mji wa Pwani wa Mombasa zinaeleza kuwa watu waliojihami na silaha walimpiga risasi Sheikh mmoja maarufu nchini Kenya Mohamed Idrissa na kupoteza maisha papo hapo.

Sheikh Mohamed Idrissa ameuawa akitoka nyumbani kwake iliyoko mtaa wa Likoni mjini Mombasa,shambulio hilo limefanyika mapema jana asubuhi.

Maofisa wa Polisi wanasema wameanza uchunguzi kwa watu waliohusika na mauaji hayo,mwezi machi mwaka huu alipigwa Sheikh Ali Bahero na kulazwa hospitalini kutokana na majeraha.

Sheikh Mohamed Idrisa na wenzake wamealaumiwa na Waislaam kutokana ushiriki wao wa kushirikiana na Serikali ya Kenya iliyowaua mamia ya Waislaam kwenye Msikiti Mussa iliyopo Majengo.

Shekhe pia alikuwa kiongozi wa kupandikizwa kwenye Msikiti wa Sakina na Serikali ya Kenya hali iliyowakasirisha waislaam wa mji wa pwani,pia anadaiwa kuchochea uvamizi na mauaji yaliofanyika Masjid Mussa yeye na baadhi ya Mashekhe wengine kwenye Baraza la Maimamu pamoja na SUPKEM waliokaribu na Serikali ya Kenya.

Ni Shekhe wa kwanza kwa upande wa Serikali ya Kenya kuawa tangu Kenya ilipo fanya uvamizi wa Kijeshi katika Ardhi ya Waislaam wa Somalia na hatimae Safu ya Mashekhe kugawanyika pande mbili ya wale walioko upande wa Serikali ya Kenya na upande uliopo Waislaam.

Mashekhe wengine waliodhihirisha haki na kupinga uvamizi wa Kenya katika Ardhi ya Somalia ni pamoja na Sheikh Al Marhuum Samir Khan,Abuud Rogo,Ibrahim Umar,na Sheikh Abuubakar Sharifi (Makaburi) wote hao waliuawa na Serikali Dhalimu ya Kenya kwa kushirikiana na Amerika na Israel.

Related Items

Update cookies preferences